You are here

Hatari Nne Za Shirika La Mashahidi Wa Jehova

Printer-friendly version

Hatari Nne Za Shirika La Mashahidi Wa Jehova

“Hoja zinazoonyesha ya kwamba shirika hili ni la uongo.”

Shirika la Mashahidi wa Yehova linajidai kuwa hilo ndilo kanisa la kweli la pekee hapa duniani. Linasema ya kwamba makanisa mengine yawe ya Katoliki au ya Kiprotestanti yote yanafunza makosa na ya kwamba yeyote ambaye si shahidi wa Yehova atauawa na Mungu. Hapa kuna sababu nne ambazo zinaonyesha ni kwa nini shirika hili linafaa kuepukwa.

1. MASHAHIDI WA YEHOVA WANAPINGA MAFUNZO MAKUU YA BIBLIA

Mashahidi wa Yehova wanapinga kuwa Yesu Kristo ni Mungu. Bali wanafunza kuwa Yesu Kristo ni malaika aliyeumbwa.

Lakini Biblia inafunza wazi wazi kwamba, Yesu Kristo ambaye ni Mwana ni Mungu. Kwa mfano Waebrania 1:8 inasema, “Lakini kwa Mwana anasema ‘kiti chako cha enzi, e Mungu, ni cha milele na milele…’ ” Vifungu vingi pia vinafunza hivi - Yohana 1:1,14; 20:26-28; Matendo ya Mitume 20:28, Warumi 9:5, Waebrania 1:3, 8-9; 2 Petero 1:1.

Mashahidi wa Yehova wanapinga kufufuka kimwili kwa Yesu Kristo. Bali wanafunza ya kwamba mwili wa Yesu uliyeyuka ukawa mvuke. Charles Taze Russell, mwanzilishi wa shirika hili alifunza, “yule mtu Yesu alikufa na amekufa milele.” (Studies in the Scriptures Vol. 5, 1899, uk. 454).

Lakini Biblia inafunza wazi wazi kwamba mwili wa Yesu ulifufuliwa: Kwa mfano Luka 24:39 - “Tazameni mikono yangu na miguu yangu. Ni mimi mwenyewe! Niguzeni na muone; roho haina mwili na mifupa kama mnavyoona nikiwa nayo.” Angalia pia Yohana 2:19-21, 20:26-28; 1 Wakorintho 15:6,14.

Mashahidi wa Yehova wanapinga kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu. Bali wanafunza kuwa Roho Mtakatifu ni nguvu tu zisizo za kibinadamu kama ile ya umeme.

Lakini Biblia inafunza wazi wazi kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu; Matendo ya Mitume 5:3-4 ‘Kisha Petero akasema, Anania, kwa nini umejazwa na Shetani moyoni mpaka ukamdanganya Mungu Roho Mtakatifu… hujawadanganya watu ila umemdanganya Mungu. Angalia pia Yohana 14:16-17, 16:13-15 Warumi 8:26-27; 2 Wakorintho 3:6,17-18; Waefeso 4:30.

Mashashidi wa Yehova wanapinga wokovu kuwa zawadi ya bure ya Mungu. Bali wanafunza ya kuwa wokovu lazima utafutwe kwa bidii na binadamu. Kuupata wokovu na kuepuka hukumu, mtu lazima ajiunge na shirika la Mashahidi wa Yehova na vilevile afanye mambo kadhaa linayoyaagiza.

Lakini Bibilia inafunza wazi wazi kwamba wokovu hauwezi kupatikana baada ya kufanya chochote - kwani hii ni zawadi ya bure ya Mungu. Waefeso 2:8-9 – “Tumeokolewa kwa sababu ya neema yake kupitia kwa imani - na hii si kwa sababu yenu bali ni zawadi ya Mungu – sio kwa matendo yetu, ili yeyote asiringe.” Angalia pia Warumi 4:1-4, Wagalatia 2:16, Tito 3:5.

Mashahidi wa Yehova wanapinga adhabu ya milele ya wenye dhambi. Bali wanafunza kwamba wenye dhambi wataangamizwa kabisa na hawataishi tena.

Lakini Biblia inafunza kuwa kutakuwa na adhabu ya milele ya wenye dhambi, Matayo 25:41,46. “Kisha atawaambia wale walio mkono wake wa kushoto, niondokeeni hapa, enyi mliolaaniwa, kwenda kwa moto wa milele uliotengenezewa Shetani na malaika wake... Basi wataondoka kwenda kwa hukumu ya milele, lakini waliotakaswa waende kwa uzima wa milele.” Angalia pia Matayo 18:8, 2 Wathesalonike 1:8-9, Ufunuo 14:10,11; 20:10,15.

Mashahidi wa Yehova wanapinga kuwa roho wa binadamu huishi baada ya kifo. Bali wanafunza kuwa, kama wanyama, maisha ya binadamu huishia kwa kifo.

Lakini biblia inafunza wazi wazi kuwa roho wa binadamu huendelea kuishi baada ya kifo: 2 Wakorintho 5:8 – “Tuna uhakika, nasema, na tungependelea kuwa mbali na mwili tuwe nyumbani na Bwana.” Tazama pia Luka 16:19-31; Wafilipi 1:23-24; Ufunuo 6:9-11.

Mashahidi wa Yehova wanafunza kuwa maisha ya milele pamoja na Mungu ni kwa wachache tu. Wanadai ya kwamba kikundi maalum cha watu 144,000 kati ya Mashahidi wa Yehova wanaweza kuokolewa na kuishi milele na Mungu mbinguni; hao wengine wataishi hapa duniani.

Lakini Biblia inafunza wazi wazi kuwa wale wote wanaoweka imani yao kwa Yesu Kristo watapata uzima wa milele pamoja na Mungu. Biblia inawataja watu hawa kuwa wengi wasiohesabika: Ufunuo 7:9, 15 – “Baada ya haya nikaangalia na mbele yangu kulikuwa na watu wengi wasioweza kuhesabika kutoka kila nchi, kabila, watu na lugha, walikuwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya mwanakondoo… wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na wanamtumikia usiku na mchana hekaluni mwake.” Tazama pia Yohana 3:15, 5:24, 12:26; Waefeso 2:19, Wafilipi 3:20, Wakolosai 3:1, Waebrania 3:1, 12:22; 2 Petero 1:10,11.

Mashahidi wa Yehova wanapinga Utatu wa Mungu, na wanafunza kuwa Shetani alizua mafunzo ya Utatu.
Hivyo basi wanatupilia mbali maandiko yoyote yanayomtambua Yesu Kristo kama Mungu na Roho Mtakatifu kama Mungu.

Lakini Biblia inafunza wazi wazi ya kwamba Mwana, Roho Mtakatifu na Baba wote ni Mungu (Yohana 1:1; 20:28, 1Yohana 5:20; Matendo 5:3, 4). Pia inafunza na kuhimiza kwamba kuna Mungu mmoja tu (Isaya 43:10; 44:6,8 n.k.) Inafunza kuwa hao watatu yaani Bwana, Mwana na Roho Mtakatifu ni Mungu mmoja. (Matayo 28:19; 1 Wakorintho 12:4-6; 2 Wakorintho 13:14; 1 Petero 1:2).

Je, si ni hatari sana kufuata shirika linalopinga mafunzo makuu ya Biblia?

2. MASHAHIDI WA YEHOVA WANACHEZEA HILA BIBLIA


Shirika la Mashahidi wa Yehova limechapisha Biblia yao wenyewe isiyo ya kweli. Biblia hii inaitwa Tafsiri ya Dunia Mpya (New World Translation). Biblia hii imejaa na mabadiliko ya vifungu vingi vya maandiko matakatifu. Mabadiliko haya yanajaribu kuficha mafunzo ya Mashahidi wa Yehova ambayo ni ya uongo na hayatokani na Biblia.

Ufananisho wa Biblia na ile danganyifu
ya Tafsiri ya Dunia Mpya
Biblia Takatifu Biblia danganyifu ya
Tafsiri ya Dunia Mpya
Yohana 1:1 — “Hapo mwanzo alikuweko Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu.”

Hili ni dhihirisho kuwa Yesu (Neno) ni Mungu.
Yohana 1:1 — “Hapo mwanzo Neno alikuwako, naye Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa mungu.

Badilisho hili lilifanywa kuunga mkono pingamizi la Mashahidi wa Yehova kuwa

Yesu ni Mungu.
Wakolosai 1:16 — “Kwa kuwa katika yeye (Yesu) vitu vyote viliumbwa… vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake.”

Haya yanafunza kuwa Yesu ni muumba wa vyote, na yeye mwenyewe sio kiumbe.
Wakolosai 1:16 — “Kwa sababu kwa njia yake vitu vingine vyote viliumbwa… Vitu vingine vyote vimeumbwa kupitia yeye na kwa ajili yake.

Neno “vingine” limeongezwa kimakosa ili kuunga mkono mafunzo potovu ya Mashahidi wa Yehova kuwa Yesu mwenyewe ni malaika aliyeumbwa.
Waebrania 1:8 — “Lakini kwa habari za Mwana asema, ‘kiti chako cha enzi, e Mungu, ni cha milele na milele.”

Tambua kwamba hapa Mungu Baba anamwita Yesu Mwana, “Mungu.”
Waebrania 1:8 — “Lakini kumhusu Mwana: “Mungu ni kiti chako cha ufalme milele na milele…”

Mpangilio wa maneno umebadilishwa na shirika la Mashahidi wa Yehova ili kuficha ukweli kuwa Yesu (Mwana) anaitwa Mungu.


Je, si ni hatari kufuata shirika linalobadilisha maandiko matakatifu.

3. MASHAHIDI WA YEHOVA WANA HISTORIA YA UNABII USIOTIMIZIKA

Viongozi wa Mashahidi wa Yehova wanadai kuzungumza kwa niaba ya Yehova Mungu kwa uwezo wa unabii lakini nyingi ya unabii wao ulishindwa kutimizika. Kwa mfano, walitabiri ya kuwa Armageddon na mwisho wa dunia ungelifanyika mwaka wa 1975. Kujaribu kuficha jambo hili, Mashahidi wa Yehova wengi hupinga ya kwamba hawakuwahi kutabiri hivi hata ingawa kuna dhibitisho katika vitabu vyao.1

Vile vile shirika la Mashahidi wa Yehova lilitabiri kuwa mwisho wa dunia ungelikuwako katika miaka ya 1914, 1915, 1918, 1925 na 1942. Walitabiri kuwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo wangefufuka na warejee duniani mwaka wa 1925. Wametabiri mambo ya uongo kila wakati.2 Biblia inatangaza kuwa utabiri wa uongo ni kionyesho cha manabii wa uongo (Kumbukumbu 18:21-22).

Je, si ni hatari kufuata shirika ambalo lina historia ya utabiri usio wa kweli?

4. SHIRIKA LA MASHAHIDI WA YEHOVA HUTUMIA MAMLAKA YAKE VIBAYA

Licha ya utabiri wa uongo, shirika la Mashahidi wa Yehova linafunza kuwa dini yao pekee ndio ya kweli, na wafuasi wao pekee ndio wakristo kamili. Linadai kuwa hakuna anayeweza kujifunza ukweli wa kiroho isipokuwa wao. Pia linafunza kuwa kuna wokovu baada ya kujiunga tu na shirika lao na kuwa kila mtu, isipokuwa Mashahidi wa Yehova, atauawa kwenye Armageddon.

Shirika la Mashahidi wa Yehova linashurutisha wanachama wake kukubali, kutii na kuitikia bila kuuliza maswali, kila amri na maelezo ya Biblia ya shirika hilo. Kwa mfano shirika la Mashahidi wa Yehova linapinga vikali upaji damu (blood transfusion). Wafuasi wa shirika hili wanatarajiwa kibinafsi kufa au kuachilia watoto wao wafe badala ya kuvunja amri hii, hata ingawa Maandiko Matakatifu hayafunzi kuwa upaji damu ni vibaya. Mshahidi wa Yehova yeyote asiyetii amri hii anaambiwa kuwa atauawa katika Armageddon inayokuja – wakati wa hukumu ya mwisho.

Kupitia njia hii, viongozi wa shirika hili hutumia woga na kuwatisha wafuasi wao ili waendelee kutii shirika lao. Viongozi wa Mashahidi wa Yehova pia wametumia utabiri wa mwisho wa dunia ili kuwatisha wafuasi wao.

Je, si ni hatari kufuata shirika linalotumia mamlaka yake kwa njia mbaya?

 



Hoja hizi nne zinaonyesha hatari za kiroho zinazohusishwa na shirika la Mashahidi wa Yehova. Pengine unashangaa, “Ni habari gani njema ya Biblia?” Zifuatazo ni hoja nne zinazoonyesha injili ya kweli ya Yesu Kristo kama inavyopatikana katika Biblia.

Jinsi ya kuwa na amani na Mungu

Ujumbe wa Biblia unaweza kufupishwa kwa hoja nne rahisi:

1. Tumetenganishwa na Mungu wa kweli na aishiye kwa sababu ya dhambi zetu.
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” Warumi 3:23.
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” Warumi 6:23.

2. Hatuwezi tukajiokoa.
“Kwa hivyo hakuna mwenye mwili atakayetangazwa kutakaswa mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kufahamu dhambi huja kwa njia ya sheria” Warumi 3:20.
“Alituokoa sio kwa sababu ya wema tulioufanya bali kwa sababu ya huruma yake.” Tito 3:5.

3. Yesu Kristo ndiye dawa aliyoitumiya Mungu kwa tatizo la dhambi zetu.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” Yohana 3:16.
“Kwa maana Kristo naye alikufa mara moja kwa ajili ya dhambi, aliyetakaswa kwa ajili yao wasiotakaswa, ili awalete kwa Mungu” 1 Petero 3:18a.

4. Lazima tumpokee Yesu Kristo kibinafsi kwa imani ili tupate kusamehewa dhambi na tupate maisha ya milele.
“Bali kwa wale wote waliompokea, na walioliamini jina lake, aliwapa uwezo kuwa watoto wa Mungu.” Yohana 1:12
“… ukimkiri kwa kinywa chako kuwa ‘Yesu ni Bwana,’ na uamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokolewa”. Warumi 10:9.
 



Ikiwa ukweli huu kutoka kwa neno la Mungu umegusa moyo wako, unaweza kukiri sasa hivi kwa kumuuliza akusamehe dhambi zako na akupatie maisha mapya katika Kristo. Ombi hili rahisi litakuongoza kuonyesha imani yako kwa Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu.

OMBI

Mwenyezi Mungu na mwenye huruma, nakiri ya kwamba nimetenda dhambi mbele zako kwa vitendo, maneno na fikira. Nimepungukiwa na wema na siwezi kujiokoa. Ahsante sana kwa kumtuma mwanao Yesu Kristo kumwaga damu yake kwa ajili yangu. Nakuomba unisamehe dhambi zangu zote, na naweka imani yangu kwa Yesu Kristo aliyenifia na akafufuka kutoka kwa wafu. Amina.
 



HOJA

1. The Watchtower, Agosti 15, 1968, uk. 499; Kingdom Ministry, Mai 1974, uk.3. Enda kwenye aya.

2. The Time is at Hand, chapisho la 1906, uk. 99, 101; The Time is at Hand, chapisho la 1915 uk. 99, 101; Pastor Russell’s Sermons, chapisho la 1917 uk. 676; The Finished Mystery, 1918, uk. 404, 485; The Watchtower, Septemba 1, 1922 uk. 262; The Watchtower, Septemba 15, 1941 uk. 288; Millions Now Living Will Never Die, 1920, uk. 88-90. Enda kwenye aya.